Msanii maarufu Koffi Olomide ampoteza mamake

Mwanamuziki wa nchi ya Congo ambaye anajulikana sana kwa nyimbo zake za Rhumba kwa lugha ya ‘Lingala’ akichanganya na ‘kifaransa’ amepoteza mamake mzazi hii leo.

Kupitiza ukurasa wake wa Facebook Koffi aliandika,

” Kwako maua, kwetu machozi. Mama leo tarehe tatu mwezi Oktoba mwaka 2020 Mwenyezi Mungu ameamua umfuate Baba, nashukuru Mungu Mama. Nakupenda sana, ndani yanguutaishi milele … Lala salama mama.”

 

 

Mama Aminata na KoffiOlomide, Congo, Rhumba

 

 

 

Koffi hakutoa maelezo zaidi kuhusu kifo cha mamake, kama alikuwa anaugua na mahali alifia. Kinachodhihirika kwa maneno yake ni huzuni kubwa.

Mama Aminata Angélique Muyonge alimleta Koffi duniani tarehe 13 mwezi Julai mwaka 1956 na akampa jina Koffi kwani alizaliwa ijumaa.

Msanii Koffi ana mashabiki wengi nchini Kenya na mra ya mwisho alikuja kwa ajili ya tamasha la muziki mambo hayakumwendea vizuri. Alionekana akimpiga teke tumboni mmoja wa wanenguaji wake jambo ambalo lilizua hamaki kati ya wakenya hasa wanawake akafurushwa Kenya.

Mwanzoni mwa mwaka alitangaza kwamba alikuwa amesuluhisha jambo hilo na serikali ya Kenya na kwamba angekuja Kenya mwezi wa tano lakini kukaja janga la Corona ambalo lilizuia safari za kimataifa na mikutano ya hadhara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *