Msamaha wa Rais

Mwanamuziki wa Marekani Lil Wayne anasemekana kuwa miongoni mwa watu ambao Rais wa taifa hilo anayeondoka Donald Trump anataka kuwapa msamaha. Mwingine anayesemekana kuwa kwenye orodha ya watakaopata msamaha wa Rais ni mwanamuziki Kodak Black kwa jina halisi Bill Kahan Kapri.

Duru zinaarifu kwamba Donald Trump alikuwa amepanga kutangaza msamaha kwa wafungwa kadhaa tarehe 19 mwezi huu wa Januari mwaka 2020 siku yake ya mwisho kuhudumu kama Rais wa Marekani.

Rais mteule wa taifa hilo Joe Biden anafaa kuchukua usukani rasmi tarehe 20 mwezi huu wa Januari mwaka 2020.

Kwa sasa Trump ameondolewa mamlakani na bunge la taifa hilo kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyovutia hata wabunge wa chama chake cha Republican na hivyo hatima ya watu hao ambao wangesamehewa haijulikani.

Kodak Black wa miaka 23 anatumikia kifungo cha miaka minne gerezani kwa tuhuma za udanganyifu wakati alikuwa akijaza fomu za kununua bunduki mara mbili mwaka 2019.

Lil Wayne naye alipatikana na kosa la kuwa na bunduki kwenye ndege ya kibinafsi mwisho wa mwaka 2019. Mwisho wa mwaka jana mahakama ilithibitisha madai dhidi yake na anastahili kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu wa Januari mwaka 2021.

Kosa hilo huenda likamletea kifungo cha miaka 10 gerezani.

Lil Wayne ana uhusiano mwema na Rais Trump na hilo lilidhihirika mwezi Oktoba mwaka jana pale ambapo taarifa za mkutano wake na Rais zilichipuza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *