Mrundiko wa taka Mlolongo wahatarisha maisha ya wakazi

Serikali ya kaunti ya Machakos imeshtumiwa vikali kwa kukosa kuzoa mrundiko wa taka katika eneo la Mlolongo.

Wakazi wa mlolongo walisema mapipa ya taka yamejaa pomoni kwa majumaa kadhaa sasa  lakini serikali ya kaunti hiyo imezembea kuyachukua.

“Mapipa haya hayajachukuliwa kwa muda wa majuma kadhaa sasa na yanatoa uvundo,” alisema mkaazi mmoja Jane Nduko.

Wakazi hao waliezea hofu ya kuambukizwa magonjwa huku wakitoa wito kwa serikali ya Machakos kuondoa mapipa hayo haraka iwezekanavyo.

“Hapo awali walikuwa wakizoa taka kwa wakati, lakini wakati huu wametukosea. Ni mwezi mmoja sasa na hawajazoa taka, tunataka serikali ya machakos iwajibike kikamilifu,” alifoka Patrick Mutua mfanyibiashara katika eneo la Mlolongo.

Wakazi hao walimlaumu gavana Alfred Mutua kwa kuzunguka kenya nzima akikusanya maoni ya wakenya huku akijiandaaa kwa uchaguzi mkuu ujao lakini ametelekeza majukumu yake katika eneo hilo.

Walimtaka gavana huyo kusikiza malalamishi yao  na kushughulikia mahitaji yao ipasavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *