Mourinho ateuliwa kocha wa AS Roma ya Italia kuanzia msimu ujao kwa miaka mitatu

Jose  Mourinho ameteuliwa kuwa meneja mpya wa  klabu ya AS Roma ya Italia kuanzia msimu ujao,wiki kadhaa baada ya kupigwa teke kutoka Tottenham Hot Spur kwa matokeo mabaya.

Mourinho aliye na umri wa miaka 58  ametangazwa kuwa meneja wa Roma msimu wa mwaka 2021/2022 akitwaa mikoba ya ukufunzi kutoka kwa Mreno mwenza  Paulo Fonseca, aliyetangaza kuondoka mapema Jumanne ifikiapo mwishoni mwa msimu huu.

Mourinho amesaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa Roma ambayo ni ya 7 ligini Italia msimu  huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *