Moses Kuria na washtakiwa wenza waachiliwa kwa dhamana ya shilingi 75,000

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria pamoja na watu wengine -29, wamekiri mashtaka yaliyohusishwa na ukiukaji kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa wa Covid-19 katika mahakama moja ya Kiambu.

Kila mmoja wao alitozwa faini ya shilingi elfu-75 au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani.

Washtakiwa hao walifikishwa Jumanne mbele ya hakimu mkuu Stella Atambo, ambapo walikabiliwa na mashtaka matano, likiwemo la kujiburudisha kwa pombe, kukosa kudumisha umbali unaohitajika baina ya watu, kukosa kuvalia barakoa, kukosa kutii maagizo yaliyoharamisha mikusanyiko ya watu na ukiukaji wa kanuni za kafyu.

Walikuwa wamekamatwa mwendo wa saa tatu usiku, katika kituo cha Havilla Cornerstone Gardens huko Karuri siku ya Jumatatu pamoja na watu wengine 19.

Polisi walipata vidokezi kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu sawia na ile ya kisiasa, jambo ambalo linakiuka kanuni za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Kiambu ni miongoni mwa Kaunti tano ambazo ziliwekewa marufuku ya usafiri huku saa za Kafyu zikianza saa mbili usiku. Pia mikusanyiko na mikutano imepigwa marufuku katika kaunti hizo.

Kaunti zingine ni pamoja na Nairobi, Machakos,Kajiado na Nakuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *