Morans wanoa makali ya mwisho kwa mashindano ya FIBA Afrobasket nchini Rwanda wiki ijayo
Timu ya taifa ya mpira wa kikapu maarufu kama Morans itafungua kampeini za kuwania kufuzu kwa mashindano ya AfroBasket dhidi ya Senegal Novemba 25 mjini Kigali Rwanda katika kundi B .
Baadae Morans watamenyana na Angola Alhmisi ijayo na kukam,ilisja ratiba dhidi ya Msumbiji tarehe 27 mwezi huu.
Wachezaji wa kulipwa na wale wa humu nchini wamekuwa kwenye kambi ya mazoezi katika uwanja wa Nyayo kwa Zaidi ya majuma mawili yaliyopita .
Timu hiyo inayoongozwa na kocha mkuu Cliff Owuor itapunguzwa hadi kusalia wachezaji 12 watakaosafiri kwa mashindano hayo ya Rwanda .
Baadhi ya wanandinga wa kulipwa walio kambini ni Desmond Owili wa kutoka Australia, Bush Wamukota aliye Rwanda na Tyler Okari kutoka Denmark .
Hata hivyo kwa mjibu wa Rais wa shirikisho la basketiboli nchini KBF Paul Otula wanakabiliwa na changamoto ya kifedha swala ambalo litatatuliwa na kamati ya watu 10 iliyoundwa kuchangisha fedha za kuisaidia timu.
“Hii kamati tumeunda ya watu 10 ambayo ina majukumu ya kuchangisha na kukusanya takriban shilingili milioni 15 zinazohitajika kwa timu hiyo”akasema Otula
Mataifa 20 yaliyotengwa katika makundi 5 ya timu nne kila moja yatashiriki mashindano ya kufuzu ya Fibaafrobasketball nchini Rwanda kati ya Novemba 24 na 29 mwaka huu.
Timu tatu bora kutoka kila kundi zitajikatia tiketi kwa mashindano ya FIBA Afrobasketball mwaka ujao nchini Rwanda.