Morans kuondoka nchini kesho kwenda Kigali kwa mashindano ya FIBA Afrobasket
Kikosi cha wachezaji 12 wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu maarufu kama Morans kitakachoshiriki mashindano ya Fiba Afrobasket mjini Kgalia Rwanda kuanzia wiki ijayo , kimetajwa huku mahodha Griffin Ligare akitemwa .
Ligare ambaye amekuwa mfungaji wa kutegemewa katika timu ya Morans amelazimika kuachwa nje kutokana na majukumu ya kikazi huku nafasi yake ikitwaliwa na mchezaji wa timu ya Kenya Ports Authority Victor Odendo.
Kikosi kilicotajwa kinawajumuisha:-
Point guard
Victor Bosire (Ulinzi Warriors)
Eric Mutoro (Ulinzi Warriors)
Shooting guards
Tylor Okari (Bakkan Bears-Denmark)
Fahim Juma (Thunder)
Victor Odendo (KPA)
Small forwards
Valentine Nyakinda (KPA)
Airel Okal (Algeria)
Fidel Owuor ( Strathmore)
Forwards
Desmond Blacio Owili (Australia)
Preston Bungei (unattached)
Ronnie Gundo( unattached)
Bush Wamukota ( Patriots Rwanda)
Morans itaondoka nchini Jumapili kuelekea Kigali huku wakifungua ratiba ya kundi B dhidi ya Senegal Jumatano ijayo kabla ya kukabana koo na Angola na kisha Msumbiji.