Mkurugenzi wa soka wa Arsenal Huss Fahmy ajiuzulu
Mkurugenzi wa soka katika kilabu ya Arsenal Huss Fahmy amejiuzulu katika harakati za timu kujipanga upya .
Fahmy aliteuliwa mwaka 2017 ili kuongeza ujuzi wa kisheria katika kandarasi za wachezaji waliopo na wale wapya wanaosajiliwa.
Hata hivyo timu hiyo imetumia hela nyingi mwaka huu katika majukumu yake ya kimataifa ikiwemo kuwatimua wafanyikazi 55 ambao hawakuwa na umuhimu na kubadilisha kitengo cha Uskauti chote hatua inayokisiwa kuchangia kujiondoa kwa msimamizi wa soka kilabuni Raul Sanllehi mwezi Agosti mwaka huu.
Arsenal intarajiwa kumwajiri mkurugenzi mpya wa saoak kuchukua nafasi ya Fahmy ingawa hatakua na usemi mkubwa ,baada ya mamlaka yake kupunguzwa.
Baadhi ya majuku ya afisi ya Fahmy yamehamishiwa kwa Edu ambaye ni mkurugenzi w akiufundi ambaye watashirikiana kwa karibu na , Arteta na meneja wa Akademia ya Arsenal Per Mertesacker.