Mkataba wa Kevin Hart na Netflix

Mchekeshaji wa nchi ya Marekani Kevin Hart ametia saini mkataba na jukwaa la kuuza vipindi na filamu kwenye mitandao ya kijamii Netflix.

Chini ya mkataba huo ataunda na pia kuigiza kwenye filamu ambayo itauzwa kwenye jukwaa hilo la Netflix.

Kampuni yake ya kuunda vipindi kwa jina “HartBeat Production” nayo imehusishwa kwenye mkataba huo.

Sasa Kevin Darnell Hart anajitayarisha kutayarisha na kuigiza kwa filamu kwa jina “True Story” na ndiyo mara ya kwanza anaigiza kwenye aina hiyo ya filamu.

Anatarajiwa kutayarisha na kuwa muigizaji mkuu kwa filamu zingine nne kulingana na mkataba huo wa miaka mingi kati yake na Netflix.

“Kushirikiana na Netflix ni fursa nzuri kwangu na kwa HartBeat nafurahia na ninashukuru Ted Sandaros na Scott Suber kwa kuniamini. Mimi nao tuna maono sawa na huwa tunawapa kipaumbele watazamaji. ” Ndiyo baadhi ya maneno ya Kevin Hart baada ya kutia saini mkataba.

Wasimamizi wa Netflix wanasema walimchagua Hart kwa uwezo wa sanaa yake ya kipekee ambayo huvutia watazamaji wa rika zote na kwamba anaweza kuwa kwa sanaa mbali mbali, kama vile vichekesho, filamu na hata vipindi vya jamii.

Kevin Hart amewahi kushirikiana na jukwaa la Netflix awali, pale ambapo alikuwa amagharamika na kuunda vipindi na kuviweka pale lakini kwa mkataba wa sasa, Netflix inalipia kila kitu kwenye mchakato mzima wa kutayarisha filamu hizo.

Kipindi chake cha vichekesho kwa jina “Zero Fucks Given” kiliwekwa kwenye Netflix miezi kadhaa iliyopita na kimekuwa kikitizamwa kwa wingi.

Bryan Smiley ambaye anafanya kazi na kampuni ya HartBeat Productions amefurahia mkataba huo akisema ni nafasi nzuri na ukurasa mpya kwao huku akitoa hakikisho kwamba wataunda filamu nzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *