Mitandao ya kijamii yazimwa huku uchaguzi mkuu uking’oa nanga Tanzania

Huku uchaguzi mkuu uking’oa nanga nchini Tanzania, watumiaji wa mitandao ya kijamii katika taifa hilo la Afrika ya mashariki walianza kupata shida za mawalisiliano kupitia mitandao ya Twitter na WhatsApp.

Kuanzia Jumanne asubuhi, watumiaji wa mtandao wa WhatsApp walikosa kupokea picha wala video.

Hata hivyo serikali haijatamka lolote kuhusu jambo hilo huku halmashauri kuu ya  kudhibiti mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) ikisalia kimya.

Watumiaji wengi wa mtandao wa WhatsApp wanaamini matatizo hayo yanahusiana na uchaguzi huo mkuu hasaa katika kisiwa cha Zanzibar.

Wakaazi wa kisiwa hicho ambacho kina aina fulani ya uhuru kujiamulia mambo, walianza kupiga kura mapema Jumanne ambapo maafisa wa tume ya uchaguzi, na wale wa usalama, waliruhusiwa kupiga kura zao.

Siku ya Jumatano watu watakuwa wakipiga kura katika eneo la Tanzania-bara na pia Zanzibar visiwani.

Rais John Magufuli anatafuta kuchaguliwa kwa muhula wa pili, huku mpinzani wake mkuu  akiwa Tundu Lissu wa chama cha Chadema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *