Mitandao ya kijamii Uganda kufungwa siku mbili kabla uchaguzi mkuu

Tume ya mawasiliano nchini Uganda imeagiza kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano ya mitandao ya kijamii kufungwa na pia utumaji jumbe, siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais ambao unakumbwa na hali ya taharuki.

Kwenye barua ambayo vyombo vya habari, mkurugenzi mkuu wa tume ya mawasiliano nchini Uganda, Irene Sewankambo, aliagiza kampuni za mawasiliano ya simu kusitisha mara moja utoaji huduma zao za mitandao ya kijamii.

Mhudumu mmoja wa sekta hiyo ambaye aliongea na shirika la habari la AFP lakini hakutaka kutajwa alisema agizo hilo lilifahamishwa kampuni za mawasiliano ya simu hii leo asubuhi.

Hata hivyo hatibu wa tume ya mawasiliano, Ibrahim Bbosa aliliambia shirika la habari la AFP kwamba hafahamu kuhusu agizo hilo.

Wakati huo huo Bobi Wine, mpinzani mkuu wa Rais Yower Museveni amesema maafisa wa usalama walivamia makazi yake na kuwapiga walinzi wawili.

Alisema uvamizi huo katika makazi yake mjini Kampala na kukamatwa kwa walinzi wake wawili kulijiri alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kituo cha redio cha Kenya cha Hot  96.

Hata hivyo polisi wamekanusha madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *