Misri waibwaga Togo na kuhatarisha maisha ya Kenya kwenda AFCON

Mabingwa mara 7 wa kombe la AFCON ,Misri walifufua matumaini ya kushiriki kipute cha mwaka 2022 nchini Cameroon baada ya kusajili ushindi wa kwanza katika kundi G wa bao 1-0 dhidi ya Togo Jumamosi usiku.

The Pharoes walijipatia bao la pekee na la ushindi katika kipindi cha pili kupitia kwa bao la kichwa la Mahmoud Hamdy akiunganisha free kick ya dakika ya 54.

Matokeo hayo yanawaweka Misri uongozini mw akundi G kwa pointi 5 sawia na Comoros watakaoikaribisha Kenya Jumapili kuanzia saa moja usiku mjini Moroni.

Ilivyo kwa sasa Kenya hawana budi kuepuka kushindwa Jumapili usiku ugenini kwa Comoros ili kuwa na mataumaini ya kufuzu kwa dimba la AFCON wakiwa na pointi 3 kutokana na mechi tatu.

Comoros nao wanahitaji ushindi dhidi ya kenya ili kuwa na uhakika wa kufuzu kwa fainali za AFCON kwa mara ya kwanza .

Katika matokeo mengine ya Jumamosi Benin wakicheza nyumbani waliwaangusha Lesotho bao 1-0 huku Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ikilazimishwa kwenda sare kapa nyumbani dhidi ya Angola.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *