Mipango ya mazishi ya mamake Koffi Olomide

Mwanamuziki wa nchi ya Congo Koffi Olomide kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii ametangaza mipango ya mazishi ya mamake.

Jumamosi iliyopita tarehe kumi mwezi oktoba mwaka huu, kulikuwa na kesha katika eneo la Saint Denis, 17 Boulevard de la Libération nchini Ufaransa.

Hata hivyo ni watu wachache walikubaliwa kuingia kutokana na sheria zilizoko za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Familia yake imekuwa ikikutana kila siku usiku katika makazi yake nchini Ufaransa.

Mazishi yamepangiwa kufanyika kesho ijumaa tarehe kumi na sita mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020 katika makaburi ya Tremblay nchini Ufaransa. Iadi ya watu itadhibitiwa wakati huo pia kwa sababu za kanuni za kuzuia kusambaa kwa Corona.

Kama njia ya kumkumbuka mamake, mwanamuziki Koffi Olomide amerekodi nyimbo mbili ambazo zitazinduliwa rasmi hiyo kesho.

Kulingana na Koffi nyimbo hizo mbili zitapatikana hata mjini Kinshasa nchini Congo kesho.

Baada ya mazishi kutakuwa na tamasha la kumkumbuka mamake Koffi Olomide katika eneo la 2 Avenue des Entrepreneurs 95400 Villiers-le-Bel.

Wakati wa kutangaza kifo cha mamake, Koffi alidondokwa na machozi kwenye video ambayo aliweka kwenye akaunti yake ya Facebook.
Mashabiki wake na hata wanamuziki wenza wamekuwa wakimtembelea ili kumfariji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *