Mgombea urais wa upinzani kisiwani Zanzibar akamatwa

Chama kikuu cha upinzani Zanzibar ACT Wazalendo, kinasema muwajiaji wake wa Urais amekamatwa.

Chama hicho kinasema Maalim Seif Sharif alikamatwa Jumanne asubuhi  mwanzoni mwa zoezi la kupiga kura mapema visiwani humo.

Kilisema mgombea urais wa chama hicho alikamatwa wakati wa kujaribu kupiga kura yake.

Zoezi la kupiga kura mapema limetengewa maafisa wa tume ya uchaguzi huko Zanzibar, maafisa wa uchaguzi na wale wa usalama.

Seif amekuwa akipinga marekebisho yaliyoruhusu upigaji kura mapema, akidai hatua hiyo inatoa mianya ya udanganyifu na makosa mengine ya uchaguzi, madai ambayo yamekanushwa vikali na tume hiyo ya uchaguzi.

Juma Saad Hamis, ambaye ni msaidizi wa kamishna wa polisi huko Pemba, alisema kwamba polisi walilazimika kutumia vitoza machozi siku ya Jumatatu wakati wa kutawanya wakaazi waliotaka kuvamia vituo vya uchaguzi.

Upizani unadai watu watatu waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya polisi kutumia risasi za moto kuwatawanya uamti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *