Mwamuzi wa Uganda William Oloya atakuwa refa wa katikati ya uwanja katika mkondo wa kwanza wa mechi ya mchujo kuwania kombe la shirikisho la soka Afrika baina ya Gor Mahia na NAPSA Stars ya Zambia Jumapili Februari 14 katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.
Oloya atasaidiwa na Waganda wenza Lee Okello atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Isa Masembe msaidizi wa pili Chelanget Ali Sabila ambaye atakuwa afisa wa nne.
Alexis Redamptus Nshimiyimana wa Rwanda atakuwa kamisaaa wa mechi hiyo huku Wycliffe Makanga,ambaye ni tabibu wa Harambee Dtars akiwa afisa wa afya kuhusu Covid 19.
NAPSA Stars ambayo ni timu wafanyikazi wa mamlaka ya malipo ya uzeeni inatarajiwa kuwasili nchini Jumatano alasiri tayari kwa mkwangurano huo.
Kogalo watamenyana na NAPSA stars anayoichezea difenda wa Harambee Stars David Owino Februari 14 kuanzia saa tisa katika uwanja wa nyayo kabla ya mechi ya marudio kupigwa nchini Zambia huku mshindi wa jumla akitinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.