Messi ampiku Ronaldo na kuwa mwanasoka aliyelipwa kiwango kikubwa cha pesa mwaka huu

Nyota wa Bercelona Lionnel Messi ndiye mwanasoka aliyelipwa kiwango kikubwa Zaidi cha pesa  mwaka huu kwa mjibu wa ripoti ya jarida la forbes.

Malipo ya  Messi ni takriban pauni milioni 97  nukta 2  akifuatwa na Cristiano Ronaldo wa  Juventus kwa pauni milioni 90 nukta 3 ,huku  Neymar wa wa Paris St-Germain na  Brazil akiwa na pauni milioni  74 nukta 1,naye  Kylian Mbappe pia wa Psg akiwa na pauni milioni 32 nukta 4  katika nafasi ya 4.

Mohamed Salah  wa Liverpool na Misri ni wa tano kwa pauni nukta 28 nukta 5,akifuatwa na Paul Pogba wa Manchester United na Ufaransa kwa pauni milioni  26 nukta 2.

Antoine Griezmann wa Barcelona anafuata kwa milioni 25 nukta  5 naye Gareth Bale wa Real Madrid na  Wales ni wa nane kwa pauni milioni 22 nukta 4 katika nafasi ya 8 ilihali  Robert Lewandowski wa Bayern Munich na  Poland kwa pauni milioni 21 nukta 6m wakati  Kipa wa Man U na uhispani  David de Gea anafunga kumi bora kwa pauni milioni 20 nukta 8.

One thought on “Messi ampiku Ronaldo na kuwa mwanasoka aliyelipwa kiwango kikubwa cha pesa mwaka huu

  • 17 September 2020 at 6:09 am
    Permalink

    Heko! Timu timamu ya Teknolojia Habari na Mawasiliano- TEHAMA

    Mungu awazidishie👏👏👏👏🥇

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *