Meneja wa zamani wa Liverpool Gerrard Houlier aaga dunia akiwa na umri wa miaka 73
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerrard Houllier ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua msururu wa magonjwa kwa takriban miaka 10 iliyopita.
Mafaransa huyo aliingoza Liverpool baina ya mwaka 1998 na 2004 na kutwaa mataji matano yakiwemo FA,League cup na mataji matatu ya Uefa 2000-2001.
Katika ukufunzi Houllier aliinza katika timu ya Le Toquet mwaka 1973 hadi 1976 kabla ya kuhamia Noex Mines mwaka 1976-1982 kabla ya kutua Lens 1982-1985 .
Mwaka 1985-1988 Houllier alikuwa na Psg kabla ya kutwikwa jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa kati ya 1988-1992.
Baadae alipandishwa cheo kuwa meneja wa Ufaransa kuanzia mwaka 1992-1993 na kuifunza Liverpool mwaka 1998-2004,na kuhamia Olympic Lyon kati ya mwaka 2005 na 2007 na kuhitimisha ukufunzi akiwa Aston Villa kuanzia wmaka 2010 hadi 2011.