Mechi ya Tottenham na Fulham yaahirishwa kutokana na Covid 19

Mechi ya ligi kuu Uingereza baina ya Tottenham na Fulham iliyokuwa ichezwe Jumatano usiku imeahirishwa kutokana na wachezaji kadhaa wa Fulham kupatikana na ugonjwa wa Covid 19.

Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wasimamizi wa ligi kuu wachezaji 18 walipatikana na Covid 19 katika ligi hiyo siku ya Jumanne baada ya kufanyiwa vipimo ikiwa idadi kubwa kunakiliwa ndani ya siku moja msimu huu .

Ni mechi ya pili kuahirishwa wiki hii kutokana na covid 19 baada ya ile ya Mancity dhidi ya Everton pia kuahirishwa Jumatatu usiku.

Kuna hofu kuwa huenda msimu huu wa ligi kuu pia ukasimamishwa endapo visa vya ugonjwa huo vitaongezeka .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *