Mchujo wa ligi kuu Fkf kuchezwa mwezi ujao

Shirikisho la soka nchini Fkf limetangaza kuwa mkondo wa kwanza wa mchuano wa kuwania nafasi moja iliyosalia katika ligi kuu utapigwa tarehe 7 mwezi ujao.

Pambano hilo litashirikisha Kisumu All-Stars iliyomaliza ya 16 katika ligi ya Kpl dhidi ya  Vihiga United iliyoibuka ya tatu kwenye ligi ya Nsl msimu jana.

Mkondo wa kwanza kuchezwa Oktoba 7 huku marudiano ikiwa tarehe 11 mwezi ujao  huku mshindi akifuzu kushiriki ligi kuu ya Fkf msimu wa wmaka 2020/2021.

Kisumu All Stars wakicheza msimu uliopita

Ligi kuu ya Fkf pamoja na ligi nyingine za soka zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa  mwezi ujao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *