Mchuano wa Ligi kuu Uingereza kati ya Newcastle na Aston Villa waahirishwa kisa Covid 19

Mchuano wa ligi kuu Uingereza Ijumaa hii baina ya Newcastle United dhidi ya Aston Villa katika uwanja wa St James Park umeahirishwa kutokana na ugonjwa wa Covid 19.

Wasimamizi wa ligi kuu Uingereza wamelazimika kufutilia mbali mechi hiyo baada ya wachezaji watano  na wafanyikazi wawili wa Newcastle  kupatikana na  virusi vya Korona wakiwa mazoezini.

Hii ni mara ya kwanza kwa mechi ya ligi kuu kuahirishwa msimu huu kutokana na Covid 19 huku tarehe mpya ya  kuchezwa kwa pambano hilo ikitarajiwa kupangwa upya.

Wachezaji na wafanyikazi wote wa Newcastle watafanyiwa vipimo vingine baadae wiki hii kubaini hatima yao na hali halisi kilabuni kuhusu Covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *