Mbosso apata kazi yake ya kwanza kama balozi

Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kama Mbosso Khan mwanamuziki anayefanya kazi chini ya kampuni ya Wasafi amepata kazi yake ya kwanza ya ubalozi.

Alhamisi tarehe 17 mwezi Septemba mwaka 2020 mwanamuziki huyo alithibitishwa kuwa balozi wa kampuni ya maziwa ya Tanga Fresh nchini Tanzania.

Kazi hiyo inahusu kutangaza bidhaa za Tanga Fresh kwa nia ya kuiongezea mauzo.

Mbosso aliyekuwa na furaha nyingi alitumia akaunti zake kwenye mitandao ya kijamii kutangaza habari hizo njema kwa wafuasi wake wapatao milioni tatu nukta nne.

Kufatia habari hizo njema Rais wa Wasafi Diamond Platinumz aliandika maneno ya kumpongeza Mbosso kwa hatua aliyoipiga kikazi.

 

Wengine kwenye familia ya Wasafi kama vile Esma Platinumz, Mama Dangote, Queen Darleen, Zuchu na Romy Jons pia walimpongeza Mbosso Khan.

Mbosso anajulikana sana kwa wimbo wake kwa jina ‘hodari’

Kazi hii mpya ya ubalozi imekuja siku chache baada ya Mbosso kukiri kwamba huwa ana tatizo la kutetemeka mikono tangu utotoni. Hawezi kushika kitu kwa muda atakiangusha. 

Kulingana naye wazazi na wakubwa zake walianza kumdhania anatumia dawa za kulevya ila kadri siku zilivyosonga wakafahamu kwamba ni tatizo la ki afya. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *