Categories
Burudani

Mazishi ya Othuol kugharimu milioni moja

Ben Maurice Onyango maarufu kama Othuol Othuol aliaga dunia jumapili tarehe kumi na moja mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020 jioni akiwa na umri wa miaka 31.

Kufikia sasa mipango ya mazishi inaendelea na kupitia mwenyekiti wa chama cha wachekeshaji nchini Ken Waudo, Othuol atazikwa tarehe 25 mwezi huu nyumbani kwao huko Ndere, Alego kaunti ya Siaya.

Kinachoshtua wengi ni gharama ya mazishi ambayo inasemekana kuwa kati ya laki saba na milioni moja.

Ken Waudo na Daniel Ndambuki

Kumekuwa na picha ya mazungumzo ya jumbe za whatsapp ambayo imekuwa ikisambazwa kwene mitandao ya kijamii inayoonyesha marehemu Othuol akiomba mtu wa pili shilingi elfu kimi na tano za matibabu na huyo mtu wa pili hampatii.

Kulingana na tangazo la mwenyekiti wa chama cha wachekeshaji, mikutano ya kupanga mazishi inafanyika kila siku kwa nyumba ya marehemu Othuol huko Kitengela na kwenye hoteli moja mjini Nairobi. Siku ya mchango itatangazwa baadaye.

Mwili wa marehemu Othuol unahifafhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Chiromo.

Marehemu Othuol amekuwa akiugua kwa muda na kulazimika kuwa ndani na nje ya hospitali mara kwa mara.

Wakati mmoja yapata miezi kumi imepita alisemekana kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu na miezi michache kabla yake kuaga dunia alithibitishwa kuwa na uvimbe kichwani.

Daniel Ndambuki almaarufu Churchill ambaye huwapa wachekeshaji jukwaa kwenye kipindi chake anasemekana kuwa nguzo muhimu katika kugharamia matibabu ya Othuol na ndiye alitangaza kifo chake kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *