Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Ghana Jerry Rawlings kufanyika tarehe 27 Januari

Serikali ya Ghana imetangaza tarehe 27 Januari kuwa siku ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Jerry Rawlings.

Mwili wa Rais huyo wa zamani utahifadhiwa katika majengo ya serikali ili kutazamwa na umma kuanzia tarehe 24 hadi 26 mwezi huu, kulingana na taarifa ya serikali ya nchi hiyo.

Rais huyo wa zamani alifariki katikati ya mwezi Novemba akiwa na umri wa miaka 73 alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Jijini Accra.

Awali, mazishi yake yalipangwa kufanywa kabla ya Kristmasi, lakini yaliahirishwa kufuatia ukosefu wa maelewano kati ya viongozi wa kitamaduni nchini Ghana.

Rawlings aliiongoza Ghana kwa karibu miaka 20 baada ya visa viwili vya mapinduzi ya kijeshi alipokuwa afisa wa ngazi za chini jeshini mwaka wa 1979 na pia mwaka wa 1981.

Pia atakumbukwa kwa kurejesha utawala wa vyama vingi nchi humo mnamo mwaka wa 1992.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *