Mataifa yaliyowasili Cameroon tayari kwa CHAN

Zikisalia siku 4   kabla  ya kuanza kwa makala ya 6 ya fainali za  kuwania kombe la CHAN  nchini Cameroon   huku mataifa 16 yakiwania kombe hilo .

Timu kadhaa zinazidi kuwasili nchini  Cameroon  tayari kwa  kipute hicho.

Wenyeji Cameroon  wamepiga kambi ya mazoezi  eneo la Mbankomo wakapokua hadi mwishoni mwa michuano hiyo

Zambia, na Uganda wamekuwa  Cameroon  kwa wiki mbili kwa sasa wakitumia mashindano ya mataifa mane kujiandaa .

Uganda Cranes imejiandaa vyema kwa kipute hicho baada ya kushinda mashindano ya kutangulia michuano hiyo walipozoa alama 7 .

Kikosi cha Cranes cha wachezaji 25 kimekita kambi ya mazoezi mjini Doula huku wakiwa kundi moja na Rwanda,Togo na .

Zambia maarufu kama  Chipolopolo, waliwasili mjini  Douala Jumamosi iliyopita na wanatarajiwa kutua mjini Limbe baadae wiki hii.

The Mena ya Niger pia wamekuwa mjini  Yaoundé kwa wiki ya pili sasa na tayari wamecheza mechi  4 wakishinda moja kupoteza 2 na kutoka sarea mchuano mmoja.

Stallions ya  Burkina Faso pia wako Cameroon kwa wiki ya pili sasa .

Mali wanatarajiwa kuwasili  Cameroon baadae Jumanne huku  Zimbabwe aikiwasili Alhamisi.

Moroko ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo walilonyakua mwaka 2017 wakiwa wenyeji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *