Mataifa 16 yatakayoshiriki CHAN 2021 kuanzia Jumamosi Januari 16

Makala ya 6 ya fainali za kombe la CHAN yataanza kutimua vumbi nchini Cameroon Jumamosi hii Januari 16 huku fainali ikipigwa Februari 7.

Kipute hiki cha kila baada ya miaka miwili huwashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani huku washiriki wa makala ya mwaka huu wakitoka maeneo yote ya bara Afrika na Togo ikiwa nchi pekee inayoshiriki kwa mara ya kwanza.

Afrika Mashariki inawakilishwa na Uganda wanaoshiriki mara ya 5,Tanzania wanaoshiriki mara ya 2 na Rwanda wanaoshiriki kwa mara ya 4.

Afrika ya kati inawakilishwa na wenyeji Cameroon waoshiriki kwa mara ya 4,Congo wanaocheza kwa mara ya 3 na DR Congo wanaoshiriki kwa mara ya 5 huku wakitawazwa mabingwa mara 2 mwaka 2009 na 2016.

Ukanda wa kaskazini mwa Afrika unawakilishwa na Libya na Moroko ambao wamenyakua kombe  hilo mara moja kila moja huku Moroko wakiwa mabingw watetezi.

Zimbabwe wakiwakilisha kusini mwa Afrika wanashiriki fainali za mwaka mwaka huu kwa mara ya 5 huku waakilishi wengine kutoka ukanda huo wakiwa Zambia inayoshiriki kw amara ya 4 na Namibia wanaoshiriki kwa mara ya 2.

Afrika magharibi Zone A inawakilishwa na Mali wanaoshiriki kw amara ya 4 na Guinea inayoshiriki kwa mara ya 3 wakati Afrika magharibi Zone B ikiwa na Burkinafasso na Niger wanaoshiriki kwa mara ya tatu na Togo wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *