Mashirika yanayokabiliana na mihadarati yatakiwa kuimarisha vita dhidi ya uraibu huo

Kamishna wa eneo la Nyanza Magu Mutindika ameagiza mashirika yote ya serikali yanayojihusisha na udhibiti wa matumizi ya pombe ya chang’aa pamoja na mihadarati katika eneo hilo kushirikiana ili kuangamiza uraibu huo ambao ni kinyume cha sheria.

Mutundika ambaye alikuwa akiongea wakati wa mkutano wa majadiliano wa wadau kwenye eneo hilo kuhusu mkutano wa udhibiti wa pombe na mihadarati katika chuo cha leba cha Tom Mboya Labour mjini  Kisumu, alisema visa vinavyoongezeka vya matumizi ya pombe na mihadarati katika kaunti ya Kisumu vimechochewa na kaunti jirani.

Aliambia kundi lake kumakinika huku nchi hii inapokaribia msimu wa sherehe na kutoa onyo wale watakaopatikana kukiuka kanuni za kukabili janga la Covid-19 kwamba watakabiliwa na sheria.

Akizungumza kwenye hafla hiyo,afisa mkuu mtendaji wa halmashauri ya NACADA Victor Okioma alizua wasiwasi kuwa pombe haramu ni tishio katika kutimiza ajenda kuu nne za serikali.

Alisema mapato mengi ya serikali yanapotea kwa njia ya kuelekeza pombe inayopaswa kuuzwa nje ya nchi kurudishwa katika soko la humu nchini na wafanyibiashara walaghai.

Okioma alitoa wito kwa mashirika ya serikali yanayohuska na utoaji wa leseni na udhibiti wa kuanguka kwa pombe haramu kuhakikisha kwamba baa zote zimepewa leseni zinazofaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *