Mashindano ya dunia ya mbio za Nyika yaahirishwa hadi mwaka 2022

Shirikisho la riadha duniani limetangaza kuahirisha mashindano ya dunia ya mbio za nyika mwaka ujao nchini Australia.

Waandalizi wa mashindano hayo Australia waliomba shirikisho la riadha ulimwenguni kuahirisha mashindnao hayo hadi mwaka 2022 kutoka na chamko jipya la ugonjwa wa Covid 19 katika taifa hilo.

Mashindano hayo ambayo yatakuwa ya makala ya 44 yaliratibiwa kuandaliwa tarehe 20 mwezi Machi mwaka ujao mjini Bathhurst Australia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *