Marekani yarejea katika mkataba wa Paris kuhusu hali ya hewa

Marekani imerejea rasmi katika mkataba wa Paris, kuhusu hali ya hewa,na hivyo kupiga juhudi za kimataifa katika kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali mpya ya Marekani chini ya Rais Joe Biden imetangaza mpango kabambe wa kupunguzwa kiwango kikubwa uchafuzi wa hewa.

Wanasayansi na wanadiplomasia wamepongeza hatua hiyo ya Marekani,huku mjumbe wa maalumu wa Marekani kuhusu hali ya hewa John Kerry akitarajiwa kushiriki kupitia mtandaoni hafla ya kuhusu kurejea kwa Marekani katika mkataba huo.

Hafla hiyo itawajumuisha mabalozi katika nchi za Uingereza na Italy,katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres na balozi wa umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa Michael Bloomberg.

Marekani ilijiondoa katika mkataba huo mwezi Juni mwaka 2017 ikitaja kuwa mkataba huo kuwa ingehujumu uchumi wa taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *