Marekani kuwaondoa wanajeshi wake nchini Somalia

Rais wa Marekani Donad Trump ameamuru kuondolewa wa karibu wanajeshi wote wa Marekani kutoka nchini Somalia, ifikapo tarehe 15 mwezi januari mwaka ujao.

Habari hizo ni kwa mujibu wa idara ya ulinzi  ya taifa  hilo. Marekani ina zaidi ya wanajeshi 700 nchini Somalia, ambao wanasaidia jeshi la nchi hiyo kupambana na kundi la kigaidi la Al Shabab na wanamgambo wa kiislamu.

Mnamo miezi ya hivi mjuzi, Trump amezungumzia  uwezekano wa taifa hilo kuondoa wanajeshi wake kutoka Iraq na Afghanistan.

Amekosoa hatua ya wanajeshi wake kupelekwa  kukomesha mizozo katika nchi za kigeni, jambo linaloigharimu nchi hiyo pesa nyingi.

Hatua hiyo inatarajiwa kutekelezwa siku chache kabla ya rais Trump kuondoka mamlakani, na inakinzana na juhudi za aliyekuwa waziri wa ulinzi aliyeachishwa kazi mwezi jana Mark Esper, mbaye alitaka idadi ndogo ya majeshi wa Marekani isalie nchini Somalia.

Mwezi uliopita wachunguzi wa serikali ya Marekani walishauri dhidi ya kuwaondoa wanajeshi hao kwani vikosi vya Somalia havitaweza kukabiliana na magaidi bila usaidizi wa Marekani.

Maafisa wa Somalia pia wamesema kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini humo kutatoa fursa kuimarika kwa makundi ya kigaidi.

Somalia imeghubikwa na msukosuko wa kisiasa kwa miongo kadhaa lakini katika miaka ya hivi karibuni, vikosi vya kudumisha amani vya Muungano wa Afrika pamoja ana vile vya Marekani vilidhibiti Jiji kuu Mogadishu na miji mingine dhidi ya Al-shabab na Al-Qaenda na washirika wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *