Marehemu George Saitoti na Joseph Nkaisery waenziwe katika kaunti ya Kajiado

Waliokuwa mawaziri wa usalama wa kitaifa Marehemu Prof George Saitoti na marehemu Joseph Nkaisery ambao ni miongoni mwa watu wa jamii ya maasai walioenziwa wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya mashujaa katika kaunti ya Kajiado.

Watu wengine  ishirini walioenziwa wakati wa sherehe hizo katika kaunty ya Kajiado ni pamoja na waliokuwa machifu wakuu waliofahamika kama  Maasai Oloiboni.

Walikabidhiwa hati za utambulisho kwa juhudi zao kwa mara ya kwanza katika kiwango cha kaunty.

Bi. Margaret Saitoti na Bi. Helen Nkaisery walipokea tuzo hizo kwa niaba ya marehemu waume wao walioaga dunia walipokuwa mamlakani  mwaka 2012 na 2017 mtawalia.

Gavana wa kaunty ya kajiado Kajiado Joseph Lenku alisema mashujaa wa kaunty hiyo wanapasa kuenziwa milele  kwa kazi yao nzuri.

Wakati huo huo,Lenku amewashutumu  baadhi ya wanasiasa kwa siasa zao za chuki ambazo huenda zikaigawanya nchi hii.

Aliwahimiza viongozi wa Kajiado waunge mkono ripoti ya BBI itakapotolewa kwa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *