Maradona alazwa Hospitalini

Gwiji wa Argentina Diego Maradona amelazwa hospitalini katika mji wa has La Plata, nchini Argentina kutokana na tatizo la ki afya ambalo halijabainika.

Kulingana na tababibu anyemuhudumia Maradona,mchezaji huyo mstaafu ni mgonjwa ila hayuko katika hatari  na atamchunguza kwa siku tatu zijazo.

Maradona  aliye na umri wa miaka 60 alikuwa uwanjani Ijumaa iliyopita timu yake anayoifunza ya Gimnasia La Plata ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Patronayo ingawa aliondoka uwanjani mechi ikianza.

Tangu astaafu kucheza mwaka  1997, Maradona ambaye amekuwa na timu za Napoli, Barcelona  na  Boca Juniors amekumbwa na msururu wa magonjwa  ikiwemo kulazwa Januari mwaka jana kutokana na kuvuja damu ndani ya tumbo  na pia alikuwa na  matatizo ya kupumua mwaka 2004 tatizo lililotakana na uraibu wa mihadarati .

Maradona anasifika kwa bao lake la “Hand of God” alilofunga kw amkono na kuisaidia  Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka 1978 nchini Mexico .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *