Maombolezo ya Gwiji wa Safari Rally Jayant Shah yaendelea

Risala za rambirambi zinazidi kumiminika kufuatia kifo cha gwiji wa mashindano ya Safari Rally nchini Jayant Shah aliyeaga
dunia Jumapili jijini Nairobi akiwa na umri wa miaka 78.
Miongoni mwa waliotoa risala zao za rambirambi ni pamoja na  mwakilishi wa shirikisho la mashindano ya magari FIA barani Afrika
Surinfer Thatthi akitaja kuwa kifo hicho ni pigo kubwa ,mkurugenzi wa kiufundi wa mashindano ya magari Afrika  Viren Goricha,
aliyemtaja kuwa rafiki wa karibu  na mwenyekiti Mombasa Motor Club (MMC) Roy McKenzie aliyesema kuwa marehemu na timu yake
ya uendeshaji magari ilikuwa na mpangilio mzuri.
Dereva huyo mstaafu  na mwenye makao yake jijini Daresalaam ,alifariki mapema jumapili baada ya kuugua kwa muda mfupi .
Jayant alitawala mashindano ya Safari Rally miaka 80 na mashindnao mengine yakiwemo  Himalayan Rally aliyoshinda mwaka 1985 na
yale ya kitaifa KNRC mara tatu mtawalia akiendesha gari aina ya  Datsun PA 10 miaka ya  1982 na 1983 na 1984 akiendesha Nissan
240RS.
Jayanta Shah akiwa mashindanoni akiendesha gari aina ya Datsun
Mara ya mwisho Jayant alishiriki mashindnao ya Guru Nanak mwaka uliopita alipomaliza wa 10  kando pia na kushiriki mashindano
kadhaa ya WRC .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *