Mancity yavunja nuksi na kufuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya tangu mwaka 2016

Manchester  City walistahimili wakati mgumu  kabla ya kuwashinda Borusia Dortmund mabao 2-1 Jumatano usiku na  kuondoa nuksi huku   wakifuzu kwa semi fainali ya kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya  kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016.

Jude Bellligham alikuwa ameiweka Dortmund uongozini kwa bao la dakika ya 15 na kudumu hadi mapumzikoni.

Hata wenyeji walizidiwa maarifa kipindi cha pili Ryad Mahrez akipachika goli la kwanza kwa Mancity kupitia penati ya dakika ya 55 kabla ya Phil Foden kuongeza la pili  dakika  ya 75.

City walitinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-2 na kuweka miadi dhidi ya PSG ya ufaransa .

Ilikuwa mara ya kwanza kwa city kufuzu kwa nusu fainali baada ya kubanduliwa katika kwota fainali mara nne mtawalia chini ya meneja Pepp Guardiola.

Guardiola pia anajiunga na Jose Mourinho kuwa makocha waliofuzu kwa nusu fainali ya ligi ya mbaingwa ulaya mara nyingi zaidi ikiwa mara 8.

Mancity wanao uwezo wa kunyakua mataji mane msimu huu ,baada ya kushinda kombe la EFL Carabao,huku pia wakikutana na Chelsea katika nusu fainali ya kombe la FA wikendi hii na pia wanaongoza ligi kwa alama 11 na pia wakiwa na fursa ya kunyakua ligi ya mabingwa ulaya.

Katika mechi nyingine Real Madrid walitoka sare tasa ugenini Anfield  dhidi ya Liverpool na kutinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

Madrid watamenyana na  Chelsea katika semi fainali nyingine ya ligi ya mabingwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *