Mamelodi na Belouizdad kuchuana Benjamin Mkapa jijini Dare salaam

Shirikisho la kandanda Afrika limetangaza kuwa mechi ya pili ya kundi B kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika kati ya mabingwa wa Ageria CR Belouizdad ya Algeria na mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns itachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Daresalaam Tanzania tarehe 28 Februari.

Mchuano huo ulikuwa upigwe mjini Algiers Algeria lakini ukalazimika kuhamishwa baada ya serikali ya Algeria kupiga marufuku safari zote za kuingia nchini humo kama njia ya kuzia msambao wa ugonjwa wa Covid 19.

Shirikishp la soka Tanzania TFF limeidhinisha pambano hilo kuandaliwa nchini humo.

CAF pia imengaza kuwa mechi ya kundi C kati ya Wydad Casablanca ya Moroko na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini itachezwa tarehe 28 mwezi Februari katika uwanja wa 4TH August mjini Ouagadogou Burkina Faso baada ya kuidhinishwa na shirikisho la kandanda nchini Burkina Faso.

Mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi kuwania ligi ya mabingwa Afrika zitapigwa kati ya Ijumaa na Jumamosi hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *