Makinda wa Uganda wahifadhi kombe la CECAFA U 17 baada ya kuwamenya Tanzania 3-1

Uganda ndio mabingwa wa komeb la Cecafa kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 baada ya kuwatitiga Tanzania mabao 3-1 katika fainali iliyochezwa Jumanne alasiri katika uga wa Umuganda Wilayani Rubavu nchini  Rwanda.

Ivan Irinimbabazi alipachika wavuni bao la Uganda Cubs kunako dakika ya 63 , naye Travis Mutyaba akatanua uongozi wa  kwa bao la dakika ya 70,  lakini Vincent Mulema wa Uganda akajifunga zikisalia dakika 2 mechi ikamilike na kuwapa Serengeti Boys wa Tanzania matumaini kwani walihitaji kuongeza bao jingine moja na kusukuma mechi kwa matuta ya penati.

Timu  ya   Uganda   ya  U 17 maarufu kama Cubs

Hata hivyo Wabongo wakisaka bao hilo moja walijisahau na kumruhusu Ibrahim Juma kupachika bao la dakika ya 91 na kuzamisha dau lao ,huku Waganda wakifahamu fika kombe ni lao  kwa mara ya pili mtawalia na kuanza shamrashamra .

Ni mara ya pili mtawalia kwa timu ya Uganda kutwaa kombe hilo la chipukizi baada ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 kunyakua kombe la Cecafa pia maajuzi nchini Tanzania.

Vijana wa Serengeti Boys kutoka Tanzania

Ethiopia iliibuka ya tatau baada ya kuwagaragaza Djibouti mabao 5-2 katika mchuano wa awali Jumanne wa kuwania nishani ya shaba katika kiwara cha Umuganda .

Kadhalika mataifa hayo ya Uganda na Tanzania yatawakilisha ukanda wa Cecafa katika michuano ya AFCON mwezi Juni mwaka ujao nchini Moroko sawia na Afcon kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 mapema mwakani nchini Mauritania.

Pia inasadifu kuwa timu za Uganda na Tanzania zitashiriki michuano ya kombe la CHAN kuanzia tarehe 16 mwezi ujoa nchini Cameroon wakisindikizwa na Rwanda.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *