Mahakama yaongeza muda wa kuzuia kuongezwa kwa ada ya kuegesha magari Nairobi

Mahakama Kuu ya Milimani imeongeza muda wa kuzuia serikali ya Kaunti ya Nairobi kuongeza ada za kuegesha magari.

Sheria hiyo mpya ina lenga kuongeza mara mbili, ada ya kuegesha magari ya kibinafsi kutoka shilingi 200 hadi shilingi 400 kwa siku.

Jaji Anthony Mrima pia alitoa uamuzi wa kuzuia kaunti hiyo kuongeza ada zinazotozwa magari ya uchukuzi wa umma.

Chama cha wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma kimesema kuongezwa kwa ada hiyo sio halali na kwamba kaunti hiyo haikuandaa vikao vya kutafuta maoni ya umma kabla kufanya uamuzi huo.

Chama hicho kinadai kuwa itawalazimu wamiliki wa Matatu kulipa shilingi 1,000 kila siku na kulalamika kwamba hatua hiyo itawapa wakati mgumu wanaohitaji kuegesha magari yao katikati mwa jiji la Nairobi.

Agizo la mahakama hiyo litadumu hadi tarehe 21 mwezi Aprili ambapo kesi hiyo itasikizwa na kuamuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *