Mahakama yaamuru kufidiwa kwa waliofurushwa kimakosa karibu na Uwanja wa Ndege wa Wilson

Zaidi ta familia elfu tatu zilizofurushwa kimakosa kutoka mtaa wa Mitumba karibu na Uwanja wa Ndege wa Wilson, sasa zitafidiwa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu.

Katika uamuzi uliotolewa kwa njia ya barua pepe, mahakama hiyo iliagiza kesi hiyo kurejeshwa katika Mahakama Kuu, ambayo itaamua kiasi cha fedha watakazolipwa.

Katika kesi hiyo, chama cha kupigania maslahi cha Mitubell kilipinga kufurushwa kwao mnamo mwaka wa 2011 na Halmashauri ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege humu nchini.

Mahakama inasema kwamba hatua hiyo ilikuwa kinyume cha agizo la mahakama, ambapo pia mali za wakazi hao ziliharibiwa.

Aidha, majaji hao walizungumzia haki ya kuwa na makaazi bora, ikizingatiwa kwamba watu hao wameishi kwa muda mrefu, na hata kujijengea nyumba na kulea familia zao kwenye kipande hicho cha ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *