Mahakama Kuu yasimamisha kwa muda kuvunjwa kwa Bunge

Wabunge wamepata afueni baada ya Mahakama Kuu kutoa agizo la muda la kusimamisha kuvunjwa kwa bunge na Rais Uhuru Kenyatta kufuatia ushauri wa Jaji Mkuu David Maraga.

Maraga alimshauri Rais kulivunja bunge kwa kile alichokitaja kama kushindwa kimakusudi kuidhinisha sheria ya thuluthi mbili ya uwakilishi wa kijinsia.

Akitoa agizo hilo, Jaji wa Mahakama Kuu Weldon Korir pia amemtaka Maraga kuteua jopo la majaji watatu kufafanua kifungu cha 261 cha katiba kuhusu utaratibu wa kulivunja bunge.

Uamuzi huo unajiri saa chache baada ya Chama cha Wanasheria nchini kutishia kuwashawishi Wakenya kukita kambi kwenye majengo ya bunge mnamo tarehe 12 mwezi ujao ikiwa Rais hatalivunja bunge hilo.

Chama hicho tayari kimeiandikia Wizara ya Fedha kuitaka isitishe mishahara na marupurupu ya wabunge kuanzia oktoba 12.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *