Magufuli na Tundu wakabana koo kwenye kinyang’anyiro cha Urais Tanzania

Raia nchini Tanzania wanatarajiwa kupiga kura leo katika uchaguzi ambao Rais Dkt. Pombe Magufuli anataka awamu ya pili ya kuliongoza taifa hilo.

Kwenye uchaguzi huo, Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi CCM, atakabiliana na mpinzani wake mkuu Tundu Lissu anayegombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Magufuli na Lissu ni miongoni mwa wagombea 15 walioidhinishwa kuwania urais na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Tanzania, mwishoni mwa mwezi Agosti.

Uchaguzi huo unafanyika wakati ambao mataifa ulimwenguni yanakabiliana na janga la virusi vya Corona na Tanzania inaingia kwenye orodha ya mataifa ya Afrika kama vile Burundi, Guinea na Mali yaliyoandaa uchaguzi wakati wa janga hilo.

Rais Magufuli aliyeingia mamlakani baada ya kushinda uchaguzi wa urais mwaka wa 2015 amepata sifa miongoni mwa raia nchini humo kwa vile alivyoshughulikia swala la ufisadi na maendeleo.

Hata hivyo, anakabiliwa na shutma kutoka kwa wafuasi wa wapinzani wanaokashifu uongozi wa serikali yake wakidai kuwa ni wa kidikteta unaowanyima wapinzani uhuru wa kujieleza.

Naye mpinzani wake mkuu Tundu Lissu katika kampeni zake amewaahidi raia wa nchi hiyo kuwa uongozi wake utakuwa wa haki kinyume na ilivyo sasa, iwapo watampa nafasi ya uongozi.

Tundu ameonekana kutofautiana na Magufuli hadharani na kumkashifu kwa maswala mengi likiwemo linsi anavyoshughulikia janga la Corona nchini humo.

Kulingana na Tundu na wapinzani wengine, Rais Magufuli aliamua kulizima swala hilo tangu mwezi Aprili ambapo alipiga marufuku utoaji wa taarifa na yakwimu za maambukizi ya ugonjwa huo, akisema kuwa nchi hiyo iko huru kutokana na COVID-19.

Hata hivyo, kumekuwa na visa ambapo madereva wa malori ya masafa marefu kutoka nchi hiyo wanapatikana na virusi hivyo wanapopimwa katika nchi jirani za Kenya na Uganda.

Kwenye uchaguzi huo, Rais Magufuli atakuwa anatarajia kuendeleza utawala wa CCM ambacho kimekuwa uongozini tangu kubuniwa kwake mnamo mwaka wa 1977.

Kwa upande wake Tundu Lissu atakuwa ananuia kuwa mgombea wa kwanza kuwahi kuking’oa mamlakani chama tawala cha CCM.

Wafuasi wa pande zote mbili wameonekana kuwa na matumaini makubwa kwa wagombea wanaowaunga mkono huku wale wa Magufuli wakitaka apewe awamu ya pili ili akamilishe ajenda zake za maendeleo, na wale wa Lissu wakihoji kuwa anapaswa kupewa nafasi ili arekebishe mianya iliyopo kwenye uongozi wa sasa.

Wapiga kura zaidi ya milioni 29 nchini humo watakuwa na nafasi ya kufanya uamuzi debeni, kuhusu atakayeongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mbali na Magufuli na Lissu, wagombea wengine ni pamoja na Leopold Mahona (NRA), John Shibuda (ADA-Tadea), Mutamwega Mgaywa (SAU), Jeremiah Magan- ja (NCCR), Cecilia Mbaga (DM), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Philipo Fumbo (DP), Bernard Membe (ACT-Wazalendo), Queen Sendiga (ADC), Hashim Rungwe (Chaum- ma), Khalfan Mazrui (UMD), Seif Maalim Seif (AAFP) naTwalib Kadege (UPDP)

2 thoughts on “Magufuli na Tundu wakabana koo kwenye kinyang’anyiro cha Urais Tanzania

  • 28 October 2020 at 6:51 pm
    Permalink

    Maneno ya mtandao haifai kuzimwa kwa njili sio itafanya sisi pigwe kama maneno ya kura ni kura na maneno mtandao ni mtandao na mbona mtandao hii ximwe whay???

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *