Magatuzi kupokea fedha zaidi baada ya Bunge la Seneti kupitisha mswada wa ugavi wa fedha

Serikali za kaunti zinatarajia kupokea, kwa mara ya kwanza, kiasi kikubwa cha mgao wa kifedha baada ya Bunge la Seneti kupitisha mswada kuhusu ugavi wa fedha kutoka hazina kuu.

Kwenye kikao mahsusi kilichofanyika jana, maseneta waliidhinisha marekebisho kwa mkataba huo jinsi ilivyopendekezwa kwenye ripoti ya bunge kuhusu fedha na bajeti.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo, mgao wa fedha kwa kaunti umeongezwa hadi shilingi bilioni 370 kutoka shilingi bilioni 316.5.

Mwaka jana Bunge la Seneti lilifikia njia panda kuhusu swala la kiwango cha mgao wa fedha kwa kaunti, huku ikidaiwa baadhi ya kaunti zitanufaika kuliko nyingine, kabla ya kufikia makubaliano ambapo kila kaunti itanufaika.

Maseneta hata hivyo wameonya serikali za kaunti dhidi ya utumizi mbaya wa fedha kufuatia ongezeko hilo la mgao wa fedha kwa kaunti.

Aidha, maseneta walionya pia kuhusu hali ya ufisadi katika ngazi za kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *