Mabingwa watetezi RS Berkane kuzindua uhasama na Kabylie ya Algeri kombe la shirikisho

Mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho la Soka Afrika RS Berkane kutoka Moroko wamejumuishwa kundi B pamoja na vigogo wa Algeria Js Kabylie kwenye droo ya kombe hilo iliyoandaliwa Jumatatu alasiri mjini Cairo Misri.

Timu nyingine kundi hilo ni Cotton Sport ya Cameroon na NAPSA Stars ya Zambia iliyoibandua Gor Mahia.

Berkane wataanza kutetea kombe hilo tarehe 10 mwezi Machi wakiwaalika NAPSA Stars,kabla ya kuzuru Yaounde kupimana nguvu na Cotton Sport ya Cameroon tarehe 17 Machi,kisha iwaalike Js Kabylie ya Algeria April 4, kuzuru Algeria kwa mechi ya marudio tarehe 11 mwezi wa nne na kisha kupiga ziara ya Lusaka kuchuana na NAPSA tarehe 25 na kuhitimisha ratiba tarehe 28 April kwa kuwaalika NAPSA.

Kundi A linajumuisha vilabu vya Enyimba kutoka Nigeria,Entete Setif ya Algeria,Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Ahli Bengazi ya Libya.

Asc Jaraaf kutoka Senegal imejumuishwa kundi C pamoja na Salitas ya Burkina Faso,CS Faxien ya Tunisia na mshindi wa mechi ya mchujo baina ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na Young Buffaloes ya Swaziland.

Pyramids ya Misri iliyoshindwa kwenye fainali ya mwaka uliopita imo kundi D pamoja na Raja Casablanca ya Moroko,Nkana Rangers kutoka Zambia na mshindi wa pambano la mchujo kati ya Premeiro de Agosto ya Angola na Namungo kutoka Tanzania.

Kombe la shirikisho Afrika

Droo kamili:-

Kundi A
Enyimba-Nigeria
Entete Setif-Algeria
Orlando Pirates-South Africa
Ahli Bengazi-Libya

Kundi B
RS Berkane-Morocco
NAPSA Stars-Zambia
JS Kabylie-Algeria
Cotton Sport-Cameroon

Kundi C
Asc Jaraaf-Senegal
Salitas – Burkina Faso
CS Faxien – Tunisia
Mshindi kati ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na Young Buffaloes ya Swaziland.

Kundi D
Pyramids – Egypt
Raja Casablanca – Morocco
Nkana Rangers-Zambia
mshindi wa pambano la mchujo kati ya Premeiro de Agosto ya Angola na Namungo kutoka Tanzania.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa dola milioni 1 nukta 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *