Mabingwa watetezi KCB waanza vyema msimu wa Kenya Cup

KCB walianza vyema harakati za kutetea taji ya cup walipowaangusha Strathmore Leos pointi 24-16 Jumamosi katika uwanja wa KCB huku msimu wa mashindano hayo ukianza rasmi.

Mjini Nakuru wenyeji Menengai Oliers waliipakata Kenya Herlequins alama 39-13 katika uwanja wa ASK Nakuru Showgrounds huku Top Fry Nakuru ikiwacharaza Blakblad ya chuo kikuu cha Kenyatta alama 13-8 katika uwanja wa Nakuru Athletic Club.

Kabras Sugar RFC walishinda derby ya Katch walipoibwaga Masinde Muliro University of Science and Technology alama 56 -0 katika
uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Kakamega .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *