Mabingwa wa Uholanzi Ajax waponzwa na Covid 19 kwa ziara ya Denmark

Mabingwa wa Uholanzi kilabu ya Ajax Amsterderm ,watalazimika kucheza mechi ya tatu ya kundi lao ya ligi ya mabingwa Ulaya  Jumanne usiku ugenini dhidi ya Midtjyaland ya Denmark   bila huduma za wachezaji 6 wa kikosi kwanza wanaougua Covid 19.

Kulingana na taarifa kutoka kwa timu hiyo ni wachezaji 17 pekee wa kikosi cha kwanza na cha pili waliosafiri kwenda Denamark kwa pambano hilo ,baada ya wachezaji 11 kupatikana na Covid 19 wakiwemo 6 wa kikosi cha kwanza.

Ajax wakichuana na Atalanta ya Itallia katika mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya

Wachezaji watakaokosa mchuano wa Jumanne ni pamoja na viungo  Ryan Gravenberch na , Davy Klaassen, nahodha Dusan Tadic, Andre Onana na  Maarten Stekelenburg huku Kjell Scherpen, ambaye hajawahijumuishwa katika kikosi cha kwanza, akiwa kipa pekee kwa mechi hiyo,  baada ya wengine wote kutengwa  kumaanisha kuwa itabidi kocha atafute mchezaji wa akiba aliye na uwezo wa kucheza langoni endapo kipa huyo atajeruhiwa au atapata kadi nyekundu.

Hata hivyo kocha Eric Ten Hag amedinda kufichua majina ya wachezaji wanaogua Covid 19 kama njia moja ya kuwalinda.

Kwa mjibu wa sheria za shirikisho la soka barani Ulaya Uefa ,mchuano unaweza kuahirishwa tu ikiwa timu ina wachezaji wanaopungua 13 wa kikosi cha kwanza.

Ajax wanawinda ushindi wa kwanza katika kundi D, baada ya kupoteza nyumbani dhidi ya Liverpool na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Atalanta katika mechi  zilizopita.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *