Mabingwa wa dunia Ufaransa wakabwa koo na Ureno

Mabingwa wa dunia Ufaransa walilazimishwa kutoka sare tasa nyumbani dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ureno katika mechi ya kundi A kuwania kombe la mataifa ya ulaya Jumapili usiku.

Timu zote mbili zilibuni nafasi chache za kufunga mabao na kuwa na asilimia sawa ya umiliki wa mpira na hadi kipenga cha mwisho timu zote zilitoka sare tasa licha ya kuwa na wachezaji bora dunia Kylian Mbape kwa Ufaransa na Cristiano Ronaldo wa Ureno.

Katika matokeo mengine ya kundi hilo Denmark walisajili ushindi wa mabao 3-0 ugenini kwa Iceland huku Poland wakilazimisha sare tasa dhidi ya Italia.

Katika kundi B Russia na Uturuki walitoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1-1,Scotland wakaingusha Slovakia bao 1 kwa sufuri huku Hungary ikiwaadhubu Serbia ugenini bao 1 -0.

Mechi hizo kuendelea kesho na Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *