Maambukizi ya Covid-19 yanazidi kuongezeka huku watu 442 zaidi wakiambukizwa nchini

Kenya  imethibitisha visa vipya 442 vya maambukizi ya Covid-19,na hivyo kuongeza idadi jumla ya maambukizi hapa nchini hadi 40,620.

Akiongea katika kaunti ya Uasin Gishu Ijumaa alipotoa taarifa ya kila siku kuhusu hali ya janga la Covid-19 hapa nchini,katibu mratibu katika wizara ya afya  Dr. Rashid Aman,alisema visa hivyo vipya vilitokana na sampuli 5,327 zilizopimwa.

Kati ya visa hivyo vipya ,419 ni Wakenya ,ilhali 23 ni raia wa kigeni.

Alisema mgonjwa wa umri mdogo ana miaka mitatu ilhali ule wa umri wa mkubwa ana miaka 86.

Dr. Aman hata hivyo alisema wagonjwa wengine wanne wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo,na kuongeza idadi jumla ya vifo kutokana na ugonjwa huo hapa nchini hadi 755.

Wagonjwa 166 wamepona ,na kuongeza idadi jumla ya waliopona hadi  30,876.

Kati ya walipona,140 walikuwa wakiuguzwa nyumbani, ilhali 26 waliruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya.

Kwa mara ya kwanza kabisa kaunti ya Nakuru imeongoza kwa maambukizi,kwa kunakili visa 94.

Aidha Dr Aman aliwatahadharisha Wakenya dhidi ya kuhudhuria mikutano ya kisiasa, akisema kulegezwa kwa masharti hakumaanishi ugonjwa huo umethibitiwa hapa nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *