Maafisa wa KWS wanasa mashua iliyotekeleza uvuvi haramu Tana River

Maafisa wa Huduma ya Wanyapori (KWS) katoka eneo la Kipini, Kaunti ya Tana River wamenasa mashua ya uvuvi ambayo ilituhumiwa kuhusika katika uvuvi haramu kwenye Bahari Hindi.

Maafisa hao wakisaidiana na wananchi na maafisa wa Kaunti ya Tana River walifanikiwa kumkamata Salim Kolombo Tawfiq, ambaye alikuwa nahodha wa mashua hiyo ya uvuvi iliyomilikiwa na Tajiri mmoja raia wa Italia.

Taarifa za polisi zimesema mashua hiyo ilikuwa ikitumia chombo cha uvuvi kilichoharamikshwa kwa uvuvi.

Chombo hicho huwaua kobe wakati wa shughuli ya uvuvi baharini kwani hakijawekwa kifaa cha kutenganisha baina ya samaki na kobe kwenye maji.

Pia kwenye mashua hiyo kulipatikana aina ya samaki aliye katika hatari ya kuangamia.

Mashua hiyo, kwa mujibu wa polisi, ilinaswa baada ya kupatikana ikipita katika sehemu ya maji ya kimo cha chini ya mita 15 ambayo ni kinyume na sheria ya bunge kuhusu uvuvi ya mwaka 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *