Maafa yaliyosababishwa na mtetemeko wa ardhi nchini Indonesia yafikia 56

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mkasa wa tetemeko la ardhi nchini Indonesia imeongezeka hadi watu 56.

Maelfu ya wakazi wa Kisiwa cha Sulawesi nchini humo wameachwa bila makao, huku shughuli za uokozi zikiendelea.

Tetemeko hilo la ardhi la makali ya 6.2 kwenye mizani ya Richa lilitokea mapema siku ya Ijumaa na kusababisha taharuki kisiwani humo.

Majengo yaliporomoka katika mji wa Mamuju, Mashariki mwa Kisiwa cha Sulawesi, ambao una wakazi 110,000.

Indonesia ilikumbwa na tetemeko jingine kubwa la ardhi mwaka wa 2018 lililosababisha vifo vya  maelfu ya watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *