Liverpool na Midtjylland kucheza mechi yao nchini Ujerumani

Shirikisho la kandanda barani Ulaya Uefa linatafakari kuhamisha mechi ya ligi ya mabingwa kati ya kilabu cha Midtjylland  kutoka Denmark dhidi ya Liverpool  hadi uwanja wa Signal Iduna Park nchini Ujerumani  kutokana na masharti makali yaliyowekwa nchini Denmark kuhusiana na msambao wa virusi vya Corona.

Pambano ambalo limeratibiwa kuchezwa Desemba 9 limekumbwa na ati ati nyingi baada ya  mshambulizi wa Liverpool Mo Salah kupatikana na ugonjwa wa Covid 19 kwa mara ya pili.

Salah alipatikana na virusi vya Corona baada ya kupimwa aliporejea timuni baada ya kuhudhuria harusi ya Ndugu yake wiki iliyopita mjini Cairo na kwa mjibu wa meneja  Klopp mshambulizi huyo ataruhusiwa kucheza Jumapili dhidi ya Liverpool  endapo vipimo vya tatu Ijumaa kubainisha hatakuwa na Covid 19.

Sheria kali zimeanzishwa nchini Denmark kuzuia watu kuingia nchini humo kama njia moja ya kuzuai maambukizi mapya ya Covid 19 ambapo wachezaji na maafisa wa Liverpool hataruhisiwa kuingia nchini humo kwa pambano hilo la mwisho la kundi lao na hivyo imewalazimu EUFA kutafuta uwanja mbadala .

Klopp atakuwa akirejea Signal Iduna Park kwa mara ya kwanza tangu aondoke baada ya kuhudumu kwa miaka 7 akiwa meneja wa timu ya Borusia Dortmund.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *