Linda wazazi! Harmonize

Harmonize mwanamuziki wa Tanzania anaonekana kuendelea kumsuta aliyekuwa rafiki yake na mkubwa wake katika ulingo wa muziki Diamond Platnumz.

Alikuwa kwenye tamasha maajuzi kisiwani Zanzibar ambapo aliimba wimbo wake kwa jina “Wapo” ambapo alihimiza waliohudhuria wawapende na kuwatunza wazazi wao.

Konde Boy alitoa wimbo huo baada ya mitandao kunung’unikia picha iliyosambazwa ya babake Diamond kwa jina Mzee Abdul akipanda gari la uchukuzi wa abiria akiwa amebeba gunia na mtoto wake anaishi maisha ya kifahari na mamake Bi Sandra.

Wafuasi na mashabiki kwenye mitandao walionekana wakimsihi Diamond amsamehe babake kwani mzazi ni mzazi. Abdul anasemekana kutelekeza Diamond na mamake Sandra na kuanzisha famili nyingine na baada ya Diamond kupata umaarufu na hela nyingi akajitokeza.

Wakati fulani baba na mwanawe walikutana na kukumbatiana wengi wakadhani kwamba yamekwisha na angemtunza mzee huyo lakini sivyo.

Kwenye wimbo wake, Harmonize ametumia maneno kama ‘Kuna watu na viatu’, ‘Mzazi ni mzazi’ na ‘kama baba na mama ndio nguzo ya dunia wapende wote sio kwamba wa kike anacheka na wa kiume analia’.

Wakati picha ya mzee Abdul ilisambaa Bi. Sandra alitetea mwanawe Diamond akisema amemfanyia mzee huyo ya kutosha na mzee naye akasema sio lazima atunzwe na Diamond na kwamba hata akifa sio lazima Diamond ahudhurie mazishi.

Harmonize aliweka wimbo huo kwenye Instagram mwisho wa mwaka 2021 akiwa nchini Ghana na kesho yake tarehe mosi mwezi Januari mwaka huu wa 2021 akaweka picha ya Diamond akimsifia na kutambua alivyomsaidia kufika aliko kimziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *