Namibia na Jamhuri ya Afrika ya kati zilitoka sare ya bao 1 katika mchuano wa mwisho wa kundi B wa mashindano ya kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 , uliopigwa katika uwanja wa Cheikha Boudiya Noukchot nchini Mauritania.
Flory Jean Michael Yangao aliiweka Afrika ya kati dakika 8 baada ya mapumziko kabla ya Penuua Kandjii kusawazisha kwa Namibia mwishoni mwa mechi na kusajili sare ya pili katika kundi hilo ,baada ya Tunisia na Burkina Faso kucheza sare tasa.
Mashindano hayo kuingia siku ya tatu Jumanne kwa mikwangurano ya kundi C ,mabingwa mara tatu Ghana watafungua dimba saa moja usiku dhidi Tanzania wanaoshiriki kwa mara ya kwanza nao Gambia wakumbane na Moroko saa nne usiku.
Mataifa 12 yanashiriki mashindano hayo .